Gavana wa Benki Kuu ya Marekani ametahadharisha kuhusu athari mbaya za vita dhidi ya Iran kwa uchumi wa Marekani na kuongezeka gharama za maisha nchini humo.

Jerome Powell amesema katika ripoti yake kuhusu makisio ya uchumi wa Marekani kwamba: Taathira za muda mrefu za vita na Iran bado hazijabainika, hata hivyo ni wazi kuwa vita hivi vitazidisha gharama za maisha nchini Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari vya Marekani, vita dhidi ya Iran vimeisababishia Marekani gharama za kijeshi za zaidi ya dola bilioni 13 katika kipindi cha wiki moja tu.

Wakati huo huo, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umetahadharisha kuhusu athari za mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kwa usalama wa chakula wa mamilioni ya watu duniani.

Naye Ghulam Reza Nouri, Waziri wa Jihadi ya Kilimo wa Iran, amwemwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) akitahadharisha kuhusu  kutishiwa usalama wa chakula kwa watu wa nchi za kanda hii kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *