Beki wa zamani wa Chelsea na West Bromwich Albion, Paul Clement anashikiliwa na Polisi nchini Hispania baada ya kukutwa akiwa na begi la bangi.

Clement mwenye umri wa miaka 47, amekamatwa katika eneo la Costa del Sol katikati ya Marbella na Fuengirola akiwa na polisi wanamtuhumu kuwa ndio alikuwa ametoka kuinunua.

Maofisa hao wa Polisi inaripotiwa wamefanya ukaguzi katika eneo la jirani na alikokamatwa na wakakuta kiasi kingine kikubwa cha bangi.

Clement aliitumikia West Bromwich kwa muda wa miaka 10 kuanzia 2000 hadi 2010 kipindi hicho ikishiriki mara kadhaa katika Ligi Kuu ya England.

Mchezaji huyo ambaye maisha yake ya soka alianzia Chelsea, ameitumikia Wet Bromwich Albion katika michezo 295 ambayo aliifungia mabao 24.

Alizuiliwa katika klabu ya bangi inayodaiwa kuwa haramu iitwayo Doobiez baada ya maafisa wa polisi kumkamata mteja aliyedai kuwa alikuwa amenunua mfuko wa bangi hapo muda mfupi uliopita.

Polisi baadaye walikamata dawa zaidi za kulevya pamoja na fedha taslimu ndani ya jengo hilo, kabla ya Clement kuonekana baadaye akitolewa nje ya jengo akiwa amefungwa pingu.

Clement, baba wa watoto wawili ambaye aliwahi kuichezea England katika ngazi za vijana, ni mdogo wa kocha msaidizi wa Brazil, Paul Clement, baadaye alifikishwa mahakamani ambapo aliachiliwa kwa dhamana akisubiri uchunguzi zaidi.

Polisi wa Hispania wamethibitisha kuwa kukamatwa kwa Clement kulifanyika Jumatatu lakini hawakumtaja hadharani mtu huyo mwenye umri wa miaka 47 aliyehusika.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu na polisi wa eneo la Mijas, ambalo Riviera del Sol ni sehemu yake, ilisema, “Polisi wa Mtaa wa Mijas wamemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kosa dhidi ya afya ya umma kufuatia operesheni iliyofanyika katika jengo lililopo katika Kituo cha Ununuzi cha Las Terrazas huko Riviera del Sol.

“Maafisa waligundua mienendo ya kutiliwa shaka ya watu waliokuwa wakiingia na kutoka katika jengo hilo walipokuwa wakifanya ufuatiliaji katika eneo hilo mchana wa Machi 10, na hatimaye walimkamata mmoja wa wateja.

“Alikutwa akiwa amebeba mfuko uliotiwa muhuri kwa joto uliokuwa na bangi, na alisema alikuwa ameununua humo ndani muda mfupi uliopita.

“Kisha walikagua jengo hilo na, baada ya kumtambua mtu anayesimamia, walikuta kiasi kikubwa cha dawa za kulevya (gramu 1,170 za bangi, gramu 865 za hashish pamoja na kiasi kikubwa cha fedha taslimu), pamoja na vifaa vilivyotumika katika kuandaa na kusambaza dawa hizo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *