#HABARI: Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa wawili wanaohusishwa na mauaji ya Athumani Nyanza, ambaye mwili wake ulipatikana ukiwa umefukiwa kwenye shimo karibu na nyumba yake Mtaa wa Kimya Kimya, Kata ya Zingiziwa, Chanika.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu Nyanza anadaiwa kuuawa na mpenzi wake, kabla ya mwili wake kuondolewa na kufukiwa katika eneo hilo ili kuficha tukio hilo.

Mashuhuda wa eneo hilo wamedai kuwa kinyume na matarajio, mauaji hayo hayakutokea nyumbani kwa marehemu, bali alichukuliwa na kupelekwa eneo jingine kabla ya kuuawa, hali iliyoongeza sintofahamu kwa wakazi wa Chanika.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *