#HABARI: Ruzuku ya pembejeo za kilimo inayotolewa na Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wakulima wadogo na vijana katika Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.

Kupitia vyama vya ushirika, wakulima wa zao la kahawa wameanza kunufaika na upatikanaji wa pembejeo kwa njia ya mikopo, hatua inayochochea ongezeko la uzalishaji pamoja na kuimarisha uchumi wa kaya.

“Kwa mara ya kwanza tulianza kufanya kazi kwa kujiorganize tu, tulikuwa tunatumia mtaji wetu binafsi lakini shughuli ilikuwa ni ngumu kwelikweli” Oscar Mwaisoloka, Mwenyekiti wa IKONONGO Entrepreneurship

Kwa mujibu wa vijana wa kikundi cha IKONONGO Entrepreneurship, msaada wa Serikali umewapa fursa ya kuachana na maisha ya kukaa mitaani na kuanza shughuli za uzalishaji, hususan katika kilimo cha miche ya kahawa.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *