#HABARI: Serikali ya Tanzania imetangaza fursa kubwa za uwekezaji katika sekta ya nishati zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 12.9 ili kukuza uchumi na kuboresha huduma za nishati nchini.

Akizungumza katika mkutano wa Powering Africa Summit jijini Washington DC, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amebainisha kuwa uwekezaji huo unahitajika katika maeneo ya uzalishaji, usafirishaji, na usambazaji wa umeme, pamoja na kukuza nishati safi ya kupikia.

Mhe. Salome ameeleza kuwa ndani ya miaka mitano ijayo, miradi 13 ya uzalishaji umeme imepangwa kutekelezwa ili kuongeza megawati 1,421, huku miradi mingine 23 ya miundombinu ikilenga kujenga kilomita 1,350 za njia za kusafirisha umeme.

Aidha, amezitaja futi za ujazo trilioni 57 za gesi asilia ambazo bado hazijatumika kikamilifu kama fursa adhimu kwa wawekezaji katika nyanja za uchimbaji na usindikaji kwa ajili ya matumizi ya viwandani na uzalishaji wa nishati.

Katika kuelekea lengo la kufikia asilimia 75 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030, serikali imewahimiza wawekezaji wa kimataifa kutumia mazingira rafiki ya biashara yaliyopo nchini kuwekeza kwenye teknolojia za kisasa.

Naibu Waziri huyo, akiambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Else Sia Kanza, amesisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inapata nishati ya kutosha, salama, na rafiki kwa mazingira.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *