Iran imethibitisha kifo cha msemaji wake wa jeshi aliyeuawa katika mashambulizi ya anga yaliyohusisha Israel dhidi ya viongozi wa ngazi ya juu wa usalama wa taifa hilo. Kifo hicho kimejiri huku mzozo wa kijeshi baina ya Israel, Marekani na Iran ukiendelea kuongezeka, na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya nishati.
Hali ya mapigano imeongeza shinikizo la kisiasa na kijeshi, huku pande zote zikionyesha kukataa kusitisha mashambulizi, jambo ambalo limechochea taharuki katika kanda ya Mashariki ya Kati na kuleta wasiwasi wa kimataifa juu ya usalama wa nishati na usafirishaji wa mali ghafi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)