
Iran iko tayari kusaidia meli za Japani kutumia Mlango-Bahari wa Hormuz, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi ameliambia shirika la habari la Kyodo News katika mahojiano yaliyochapishwa leo Jumamosi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Japan inategemea sana uagizaji wa mafuta ghafi kutoka Mashariki ya Kati, ambayo mengi hupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya biashara kwa usambazaji wa mafuta duniani.
Iran imezuia ufikiaji wa mlango-bahari huo kutokana na mashambulizi ya Israel na Marekani, na kuziacha nchi zinazotegemea njia hii ya maji zikijitahidi kutafuta njia mbadala na kutumia akiba zao.
“Hatujafunga mlango-bahari. Uko wazi,” Araghchi alidai katika mahojiano ya simu na shirika la habari la Kyodo News siku ya Ijumaa. Kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, nchi zinazoshambulia Iran zinakabiliwa na vikwazo, lakini zingine zinapewa msaada.
Nchi tano za Kiarabu zinalaani mashambulizi ya Israel nchini Syria
Wakati huo huo Saudi Arabia, Misri, Qatar, Jordan, na Kuwait zimelaani mashambulizi ya Israel kusini mwa Syria siku ya Jumamosi. “Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia inaeleza kwamba serikali ya Saudi Arabia imelaani uchokozi wa wazi wa Israel unaolenga miundombinu ya kijeshi kusini mwa Jamhuri ya Kiarabu ya Syria, katika ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na uhuru wa Syria,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi imesema katika taarifa. Misri, Qatar, Jordan, na Kuwait zilijiunga na Saudi Arabia zikisisitiza hitaji la kuhakikisha uhuru wa Syria na jukumu la jumuiya ya kimataifa katika kuzuia mashambulizi kama hayo.