Shirika la nguvu za Atomiki la Iran (AEOI) limethibitisha Marekani na Israeli kushambulia tena kituo chake cha nyukiia cha Natanz.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake shirika hilo limesema baada ya ukaguzi wa kiufundi kwenye kituo hicho, wataalamu wamebaini kuwa hakuna mionzi iliyovuja na kwamba raia wanaoishi kuzunguka eneo hilo hawako hatarini.

Shirika hilo limelaani mashambulio hayo, likisema ni ukiukaji wa wazi wa mkataba wa kimataifa kuhusu nyuklia pamoja na kanuni nyingine za usalama wa urani.

Mwezi Juni mwaka uliopita, Marekani iliangusha mabomu kwenye vituo vitatu vya nyuklia vya Iran, ikiwa ni pamoja na Natanz, Fordo na Isfagan, mashambulio ambayo baadae rais Donald Trump alidai program zote za nyuklia za Iran zilikuwa zimeharibiwa.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesisitiza kuwa nchi yake hailengi kumiliki silaha za nyukilia kama inavyodaiwa na Marekani na Israeli na kwamba kiongozi wa zamani wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliwaambia kwamba matumizi ya silaha za nyukilia ni haram.

Soma piaHatujawahi taka kuwa na silaha za nyukilia kama inavyodaiwa : Iran

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *