
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Kenya (KMD) imesema mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi imesababisha mafuriko makubwa na kusababisha vifo vya watu 81 ndani ya mwezi huu.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, mvua hizo zinaendelea kunyesha katika sehemu nyingi nchini humo huku kanda ya Magharibi ikiathirika zaidi. Taarifa zinasema kuwa baadhi ya maeneo ya vijiji katika Kaunti ya Kisumu vimezamishwa na maji huku zaidi ya hekari 1,200 za mashamba zikiharibiwa na kusombwa na mafuriko.
Mpaka sasa zaidi ya familia 3,000 zimelazimika kuhama makazi yao katika eneo la Nyakach ambapo baadhi yao wamepata hifadhi katika vituo nane vilivyoandaliwa kusaidia waathirika. Hatahivyo, maji yanayomwagika kutoka Mto Mirui yanaendelea kutishia usalama wa raia katika maeneo hayo.
Hadi sasa mji mkuu wa Nairobi ndio ulioripoti idadi kubwa ya vifo ambapo watu 37 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko. SOMA: ‘Tumieni taarifa sahihi za hali ya hewa’