Mtoto ajinyonga kisa kukanywa na wazaziMtoto ajinyonga kisa kukanywa na wazazi

POLISI mkoani Morogoro wanachunguza kifo cha Rajabu Ally Mohammed (12), mtoto wa nyumbani na mkazi wa Ijava, Kata ya Italagwe, Wilaya ya Gairo aliyekutwa amejinyonga nyuma ya nyumba yao kwa kutumia mkanda wa suruali.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Alex Mkama amesema tukio hilo lilitokea asubuhi ya Machi 23, 2026, katika Kitongoji cha Kaloleni, Kata ya Italagwe. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa siku ya Machi 22, Rajabu alikemewa na wazazi wake kuacha vitendo vya udokozi baada ya kukamatwa akiwa na wenzake wawili wakiwa wameiba mahindi mabichi.

Kamanda Mkama amesema kitendo cha kukemewa kilimjaza hasira na kumfanya mtoto huyo kujiua. Kufuatia tukio hilo, Kamanda Alex amewataka watoto wote mkoani humo kusikiliza mafundisho ya wazazi, walimu na viongozi wa kijamii ili kuepuka tabia mbaya zitakazoweza kuwapelekea kupoteza maisha. SOMA: Binti darasa la nne adaiwa kujinyonga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *