Nchini Uganda, Mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali ya Haki za Binadamu yanalaani kusitishwa kwa shughuli kao na kufungiwa kwa akaunti zao za benki. Wiki iliyopita, mamlaka ilifungia akaunti za Benki za mashirika kadhaa kama sehemu ya uchunguzi kuhusu ufadhili wao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mashirika hayo ni Chapter four uganda, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi kuhusu utawala na haki za binadamu. Hii inakuja kukiwa na mvutano mkubwa baada ya uchaguzi wa rais mwezi Januari mwaka huu.

Hatua hizi zilizochukuliwa na mamlaka za Uganda zinakuja kufuatia ukandamizaji wa serikali, ambayo inashutumu baadhi ya mashirika kwa kuhudumia maslahi ya jje na imeongeza hatua za kusitishwa kwa shughuli za mashirika hayo tangu uchaguzi wa mwezi Januari.

Kwa mashirika haya yasiyo ya kiserikali, athari zimeanza kujitokeza kufuatia hatua hizo. Paul Wasser, Mjumbe wa Chapter four uganda, Amezungumza na Christina Okello wa RFI.

“Kwa sasa, hatuwezi kufanya Kazi tena. Ofisi Zetu Zimeendelea Zimefungwa. Hatuwezi Kuwalipa wafanyakazi wetu au kulipa kodi.” Hatuwezi kufanya tena kazi kisheria. Katika hatua hii, hakuna ushahidi madhubuti uliowasilishwa kwetu. Nadhani Tunalengwa tu kwa sababu ya kazi tunayofanya.”

“Kazi hii inahusu utetezi wa haki za binadamu, utawala, na michakato ya kidemokrasia,” anaelezea Paul Wasser. “Na nina hisia kwamba inakuwa mada mwiko nchini, haswa kwa kuwa mashirika kadhaa yanayofanya kazi katika nyanja hizi pia yamelengwa.”

“Huko nyuma mnamo mwaka 2021, shirika letu lilifungwa na ofisi inayosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali. Kusitishwa huko kulidumu kati ya miezi minane na kumi,” ameongeza. “Wakati huu, hatua hii inatumika tangu Januari 13. Tunachoomba ni uwazi katika mchakato mzima na kuweza kuendelea na shughuli zetu. Hatujavunja sheria yoyote. Tunaamini hatutishii usalama. Kukemea ukosefu wa haki haipaswi kuwa uhalifu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *