Nchini Burkina Faso, wanajeshi wa Burkina Faso na washirika wao (VDP) wamekabiliwa tena na shambulio la wanajihadi kutoka Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM). Shambulio la hivi karibuni lilitokea siku ya Jumapili, Machi 22, katika mkoa wa Kaskazini-Kati na kusababisha vifo vya watu wasiopungua ishirini.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, yenye tarehe ya Jumapili, Machi 22, inaonyesha wanajeshi wa Burkina Faso wakiandamana na kujisifu kuhusu kuchoma vibanda zaidi ya kumi katika kijiji kimoja. Wanaelezea kambi iliyoko msituni karibu na mji wa Tougouri, katika mkoa wa Kaskazini-Kati wa Burkina Faso, kama mahali wanakojihifadhi wanajihadi.

Ushindi huu ambao haukutarajiwa uligeuka haraka kuwa hasara kwa upande wa jeshi na washirika wake, kwani baadaye siku hiyo, kikosi hicho kilivamiwa na magaidi, ambao hawakuonyesha huruma kwa maadui zao.

Katika video nyingine, wakati huu iliyorushwa na wanajihadi wa JNIM, mmoja wa wanajeshi waliowasha moto anaonekana akipigwa risasi akiwa amelala chini, huku washambuliaji wakikagua begi lake la kijeshi.

Wanajihadi hao ndio waliowarekodi wanajeshi hawa waliouawa kinyama, ambao baadhi yao miili yao ilichomwa na magaidi wa JNIM, ambao walidai kuhusika katika taarifa kwa Kiarabu kwa kuwaua watu zaidi ya ishirini na kuwanyang’anya silaha, vifaa, na simu za mkononi.

Magaidi hawa wanadhibiti eneo la Yagadi, zaidi ya kilomita 150 kutoka Kaya, mji mkuu wa kanda ya  kwanza ya kijeshi nchini Burkina Faso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *