
Baraza la nchi wanachama za Umoja wa Mataifa, hivi leo litapiga kura kuhusu azimio lililowasilishwa na Ghana kuhusu kutambua biashara ya utumwa barani Afrika kama ‘uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu’, azimio ambalo wanaharakati wanasema ni njia ya kuelekea uponyaji na haki.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Ghana, John Mahama, mmoja ya viongozi wa Afrika ambaye amekuwa mstari wa mbele kupigia chapuo suala la fidia kwa wahanga wa biashara hiyo, alizuru makao makuu ya umoja wa Mataifa hapo jana kuzishawishi nchi wanachama katika tukio hili la kihistoria.
Rais Mahama, amewaambia wajumbe kuwa, azimio hili litaruhusu jumuiya ya kimataifa kuwajibika na kuwa mashahidi kwa wanawake, wanaume na watoto tu zaidi ya milioni 12.5 ambao jamii zao, majina, familia, ndoto, matumaini na maisha zilidhulumiwa katika kipindi cha miaka 400 iliyopita.
Rais Mahama alizinyooshea kidole nchi ambazo zinajaribu kuficha historia ya utumwa wa Afrika, ikiwemo Marekani ambayo hivi karibuni ilipiga marufuku vitabu vya historia ya utumwa ili watoto wasijue ukweli.
Licha ya upinzani toka kwa baadhi ya nchi, bara la Afrika limepata uungwaji mkono wa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, pamoja na nchi za Carribean.