Jenerali mstaafu wa Marekani amezungumzia mashinikizo ya kiuchumi na kisiasa yanayoongezeka kwa serikali ya Washington kutokana na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, na kukiri kwamba Wairani wanaweza “kukabiliana na mashambulizi haya kwa miaka mingi.”

Jenerali mstaafu wa Jeshi la Marekani James Spider Marks, akizungumza na mtandao wa habari wa MS Now, amekiri kwamba Iran inaweza kustahamili mashambulizi ya Marekani na Israel, akibainisha kuwa operesheni hii ina “gharama kubwa” kwa serikali ya Marekani. Amesema: Trump anakabiliwa na machaguo mawili; anaweza kuendelea na uvamizi huu “wenye gharama kubwa” na wenye matokeo mabaya ya kisiasa au kujaribu kupata aina fulani ya suluhisho la kidiplomasia.

Jenerali huyo mstaafu wa Marekani amesema: “Ninaamini Iran haitasalimu amri na haitarudi nyuma. Wanajitoa mhanga lakini hawatasalimu amri na wataendeleza mapambano; Nadhani wanaweza kuendelea kusimama kidete kwa miaka kadhaa.”

Jenerali huyo wa Marekani amekiri kwamba kwa sababu ya mashinikizo yanayoongezeka kutokana na athari mbaya za kiuchumi za vita, Trump ameonyesha dalili za hamu ya kutumia mbinu ya kidiplomasia ya kukomesha vita vya sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *