
Makombora ya Qadir ya baharini ya Jeshi la Wanamaji la Iran yameshambulia kundi la meli za kivita za Marekani linaloongozwa na manowari ya Abraham Lincoln na kulilazimisha kukimbia na kubadilisha eneo lake.
Admirali Shahram Irani, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, ambaye binafsi alitoa amri ya kufyatua kombora hilo dhidi ya meli ya USS Abraham Lincoln kutoka makao makuu ya operesheni ya jeshi, amewakumbuka na kutoa heshima kwa mashahidi wa meli ya Dena na kusema: “Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, likiwa na utashi thabiti na kudhibiti kikamilifu maeneo ya baharini katika Ghuba ya Uajemi na Mlango-Bahari wa Hormuz, huku likifuatilia harakati za meli za kijeshi na maadui kaskazini mwa mzunguko wa digrii ya 10, halitapumzika hadi tutakapolipiza kisasi cha damu ya mashahidi wetu wapendwa.”
Admirali Irani ameongeza kuwa: “Kama Mlima Dena, tunasimama imara kwa ajili ya fahari na utukufu wa Iran na Wairani, na tutakuwa tumaini la wanaokandamizwa na mwiba katika jicho la adui.”
Admirali Shahram Irani ameongeza kusema: Utendaji na mienendo ya manowari ya adui ya Abraham Lincoln inafuatiliwa daima na Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na mara tu meli hizo za adui zitakapokuwa ndani ya masafa ya makombora yetu, zitakuwa shabaha ya mashambulizi makali ya Jeshi la Wanamaji.