Sergei Shoigu Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia amesema: Mashambulizi yasiyo na sababu ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni hujuma dhidi ya mfumo wa usalama wa kanda na kimataifa.

Sergei Shoigu ameeleza kuwa mashambulizi hayo ya kijeshi si tu ni hujuma kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bali kwa mfumo wote wa usalama wa kikanda na kimataifa. “Juhudi za miaka kadhaa za kuipatia ufumbuzi kadhia ya miradi ya nyuklia ya Iran zimepotea’, amesema Shoigu. 

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Johann Wadephul ameyataja madai ya Rais Donald Trump ya kufanya mazungumzo na Iran kuwa hatua muhimu na akasema kwamba kunapasa kupatikana njia ya kukomesha vita dhidi ya Iran. Wadephul amesisitiza: “Kuna jambo linaendelea.”

Mashambulizi ya pamoja ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalianza Februari 28, 2026. Hujuma hiyo ilifanywa huku mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yakiendelea kwa upatanishi wa Oman.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *