Wakazi wa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wana wasiwasi wakati bwawa lililoko kusini-magharibi mwa jiji liko katika hali ya hatari ya kuporomoka. Katika taarifa iliyotolewa wiki hii, Mamlaka ya Rasilimali za Maji ilionya kwamba miundombinu iko katika kiwango cha juu kutokana na mvua kubwa ambayo imenyesha katika mji mkuu katika wiki za hivi karibuni. Inawaomba wakazi wa vitongoji sita jijini humo kuhama. Kitongoji duni cha Kibera ni miongoni vitongoji hivyo.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Nairobi, Gaëlle Laleix
Agizo la uokoaji linahusu eneo la CDC Mtoni huko Kibera. Nyumba za bati huko zimejengwa kwenye kingo za Mto Nairobi, katika mji mkuu wa Kenya. Nyumba ya Helena ilikumbwa na mafuriko wiki chache zilizopita. “Maji yaliingia ndani ya nyumba yangu na kusomba kila kitu. Ilinibidi nianze upya maisha nikiwa nimepoteza kila kitu. Tulihamia hapa.” Ni karibu pia na mto, lakini juu kidogo. Zaidi tena, kodi ya nyumba iko ni ghali. Sina uwezo.”
Helena hulipa shilingi 2,000 kwa mwezi, sawa na euro 13, kwa kibanda chake cha bati cha mita za mraba chache. Kwa upande mwingine, Phoebe alihamia mita 300 kutoka makazi yake ya zamani yaliyoharibiwa na mafuriko. Na analipa karibu mara mbili, kwa usalama zaidi. “Ninaogopa. Hatujui nini kinaweza kutokea ikiwa bwawa litavunjika. Mahali ambapo nina duka langu si rahisi kpata sehemu nyinngine. Ndiyo maana ninakaa hapa, ili kuendelea na biashara yangu. Ni hatari, lakini Kibera ndo hivo, mtu unahatarisha maisha yako kwa ajili kuishi.”
Kila mita 100 kutoka mto, kodi huongezeka kwa karibu shilingi 1,000. Kulingana na Caren Akinyi Nyonje wa Kituo cha Haki ya Jamii cha Kibera, mvua zimesababisha bei kuongezeka zaidi. “Wamiliki wengi wa nyumba wameongeza kodi kwa sababu wanajua watu wanahitaji sana nyumba. Ni biashara kwao. Gavana Sakaja anazungumza lakini hayupo uwanjani. Unawezaje kuwaambia watu wahame bila kuwatafutia suluhisho?”
Hofu inaongezeka kuhusu bwawa la Nairobi
Bwawa la Nairobi lilijengwa mwaka wa 1953. Kkulingana na gavana wa jiji, miundombinu hii ya kuzeeka sasa ni hatari. “Ikiwa bwawa la Nairobi litavunjika leo, watu wengi watapoteza maisha. Kwa hivyo katika nyakati kama hizi, wakati maisha yapo hatarini, lazima tufanye yaliyo sawa. Sio ishara ya kisiasa. Na kisha tutatatua tatizo hili ambalo limekuwa likiendelea kwa zaidi ya miaka thelathini.”
Peninnah anaishi katika kitongoji cha CDC Mtoni cha Kibera. Nyumba yake iko mita mia chache kutoka Mto Nairobi. Licha ya hatari hiyo, Penina na watoto wake wanne wanabaki katika nyumba yao ya bati. “Hapa, hatuko salama sana. Inaponyesha mvua, maji huingia ndani ya nyumba, lakini sina uwezo wa kifedha kwenda mahali pengine popote. Mimi husafisha nyumba hapa na pale; Siwezi kumudu kitu chochote bora zaidi ya nyumba hii. Inauma kwa sababu nina watoto na hakuna mahali pengine pa kwenda.”
Mbele kidogo ya barabara, jirani yake Berryl pia ana wasiwasi. Tayari alikubwa na mafuriko mwaka jana. Ili kuhama, ilibidi achukue mikopo kutoka kwa kanisa lake na jamaa. “Ndiyo, nina wasiwasi kwa sababu tuna hatari ya kuathiriwa hapa pia. Nyumba yangu imejengwa kwa matofali ya matope, ingawa iko juu kidogo, kwenye ukingo wa mto. Wanapaswa kutangaza mafuriko kuwa janga la kitaifa. Bila msaada, hatuna chochote, tunasubiri yatakyotokea, hatuwezi kuhama.”
Mnamo mwaka 2024, kuanguka kwa bwawa huko Gachie, nje kidogo ya Nairobi, kulisababisha vifo vya watu wapatao thelathini katika kitongoji duni cha Mathare, chini ya mto. Tangu kuanza kwa msimu wa mvua, mafuriko yamesababisha vifo 81 kote nchini.