Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Arusha imeanzisha operesheni maalum ya kudhibiti bodaboda zinazokiuka sheria, zikiwemo pikipiki zenye kelele za milipuko na taa zenye mwanga mkali, ili kuimarisha usalama barabarani na kupunguza kero kwa wananchi.
Akizungumza katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Dkt. Jacob Rombo, amesema hatua hiyo inalenga kulinda usalama wa watumiaji wa barabara huku akiwataka waendesha bodaboda kuacha mara moja uharibifu wa mifumo ya pikipiki.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha, SSP Georgina Matagi, amesema ndani ya operesheni hiyo, pikipiki 248 zenye taa kali na 13 zenye kelele za mlipuko zimekamatwa.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)