
Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetangaza utekelezaji wa wimbi 83 la Operesheni Ahadi ya Kweli- 4 mapema leo Ijumaa, kikilenga vituo muhimu vya kijeshi vya Marekani na Israel kote katika eneo la Asia Magharibi kwa makombora na ndege zisizo na rubani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma ua IRGC, operesheni hiyo imetekelezwa kwa niaba ya “watu wema wa ukanda wa kusini mwa nchi kaskazini mwa Ghuba ya Uajemi” na imefanyika kwa kaulimbiu takatifu “Ya Aba Abdillah Al-Hussein (AS).”
Mashambulizi hayo yamelenga vituo na ngome mbalimbali za kimkakati zinazomilikiwa na vikosi vya majeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni.
Miongoni mwa shabaha zilizolengwa katika wimbi la sasa la Operesheni Ahadi ya Kweli-4 yalikuwa matangi ya kuhifadhia mafuta na ghala la mafuta huko Ashdod, makazi ya wanajeshi wa Israel katika kitongoji cha Modi’in na kituo cha kubadilishana taarifa za kijeshi cha Marekani katika kanda ya Asia Magharibi.
IRGC pia imeshambulia kambi za kijeshi za Marekani huko Al-Dhafra Umoja wa Falme wa Kiarabu (UAE) na Al-Udeiri nchini Qatar, pamoja na maeneo ya matengenezo na uhifadhi wa ndege za usafiri na ndege zisizo na rubani katika Kambi ya Anga ya Ali Al-Salem nchini Kuwait.
IRGC poa imlenga matangi ya mafuta ya ndege za kivita na ndege za vikosi vya majeshi ya Marekani, pamoja na hangari ya matengenezo na ukarabati wa mfumo wa makombora wa Patriot katika Kituo cha Sheikh Isa huko Bahrain.
Taarifa ya IRGC imeeleza kuwa operesheni hiyo ilitumia mseto wa silaha za kisasa, ikiwa ni pamoja na mifumo ya makombora ya masafa marefu na ya kati, makombora yanayotumia fueli mango na ya kimiminika, uwezo wa kushambulia kwa usahihi, pamoja na ndege zisizo na rubani za kamikaze.
Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imeongeza kuwa: Mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi yamefanyika kwa “mafanikio kamili kwa baraka Zake Mwenyezi Mungu.”
Katika taarifa yake, IRGC iliangazia athari za operesheni ya sasa kwa maisha ya kila siku kwa walowezi wa Israel, ikibainisha kwamba “maisha yanayoambatana na vingora na kufungwa kwa muda mrefu katika mahandaki ya chini ya ardhi yamekuwa utaratibu wa kila siku kwa Wazayuni.”
IRGC ilihitimisha kwa onyo kali: “Kama tulivyosema, tutawapata, na kwa matakwa ya Mungu, tutawalipa jazaa kwa matendo yenu maovu.”