NAIROBI – Rais wa Djibouti, Ismaïl Omar Guelleh, amezindua ujenzi wa nyumba za kisasa za bei nafuu zipatazo 7,000 katika jiji la Salaam, huu ukiwa mradi mkubwa wa nyumba kuanzishwa na serikali ya nchi hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ni mradi unaoendelezwa na kampuni ya uwekezaji ya Salaam Real Estate, na utagharimu dola milioni 480. Salaam City imeundwa kuendana na wakati wa sasa, kwa mujibu wa meneja mkuu wa Salaam Real Estate, Mustafe Liibaan.

Ni mradi ambao unatekelezwa kwa awamu chini ya miaka mitano ambapo wakazi wa kwanza wanatarajiwa kupewa nyumba hizo kufikia mwaka 2028. Ni mradi pia ambao unatarajiwa kuchochea kuimarika kwa uchumi wa Djibouti, ambapo wafanyakazi zaidi ya 2,000 wataajiriwa eneo hilo.

Ramani ya jiji la Salaam Real Estate, nchini Djibouti
Ramani ya jiji la Salaam Real Estate, nchini Djibouti © Djibouti

Benki ya Salaam Africa ndiyo mfadhili mkuu wa mradi huo ambapo meneja wake Djama Hersi, amesema lengo lao kuu ni kuwasaidia raia wa kipato cha chini kupata uwezo wa kumiliki nyumba za kisasa na za bei nafuu.

Muongo uliopita, Djibouti imewekeza kwa kiasi kikubwa katika bandari, reli na miundombinu ya usafirishaji kama sehemu ya mkakati wa ruwaza ya mwaka 2035 unaolenga kubadilisha uchumi wa taifa hilo la pembe ya Afrika.

Ikiwa karibu na mlango wa bahari wa Bab el-Mandeb, mojawapo ya njia zenye shughuli nyingi zaidi duniani zinazounganisha Bahari ya Shamu na Bahari ya Hindi, Djibouti imeibuka kama eneo muhimu kati ya Afrika, Mashariki ya Kati na njia za biashara za kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *