
Kulingana na ripoti zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya Mauritania na kuthibitishwa kwa RFI na vyanzo vya usalama vya Mauritania na Mali, doria ya jeshi la Mali iliingia katika vijiji kadhaa katika wilaya ya Gogui, katika eneo la Hodh El Gharbi, siku ya Jumatano asubuhi, Machi 25.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mpaka kati ya nchi hizo mbili haujawekwa wazi katika eneo hili. Uvamizi huu unafuatia matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakichochea mvutano mkubwa kati ya Mali na Mauritania kwa siku kumi zilizopita, ambao Nouakchott inajaribu kuudhibiti.
Shirika la habari la Mauritania Al Akhbar na tovuti ya Saharamedias, yakimnukuu meya wa Gogui na vyanzo vingine vya ndani, yanaripoti kwamba wanajeshi wa Mali waliingia katika vijiji kadhaa ndani ya wilaya hii na kudai kwamba bendera ya Mauritania iliyokuwa ikipepea juu ya shule katika mojawapo ya vijiji hivi iondolewe. Baada ya wakazi kpinga hili, wanajeshi wa Mali hatimaye waliondoka.
Wanajeshi wa Mali waondoka bila vurugu
Taarifa hiyo ilithibitishwa kwa RFI na chanzo cha usalama cha Mauritania, ambacho kilibainisha kuwa doria ya Mali ilikuwa na magari manne yenye silaha, na kwamba wanajeshi waliondoka bila vurugu yoyote, baada ya kurekodi viwianishi vya GPS. “Kwa kweli kulikuwa na uvamizi,” chanzo cha usalama cha Mali kilithibitisha, “lakini katika eneo hili, wanajeshi wa Mali walichanganyikiwa. Walidhani wako katika ardhi ya Mali. Kisha, waliombwa kuondoka na viongozi wao.”
Tukio hilo halijawa mada ya taarifa yoyote rasmi. Ikiwasiliana na RFI, Wizara ya Mambo ya Nje ya Mauritania haikuthibitisha wala kupinga tukio hilo, na jeshi la Mali na Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali hawakuzungumza chochote.
“Uchochezi”
Katika eneo hili, hmpaka haujawekwa vizuri. Hapo awali, Mali na Mauritaniazilichukua hatua za kutekeleza vyema sera hii.
Kufuatia mauaji ya wachungaji wawili wa Mauritania huko Mali, karibu na mpaka, siku ya Ijumaa, Machi 20, na kipindi cha kutoroka kwa mateka wa Mali waliokuwa wakizuiliwa nchini Mauritania wiki iliyopita, uvamizi huu unaonekana na waangalizi kadhaa wa Mauritania kama “uchokozi” mpya.
Siku ya Jumatatu, Machi 23, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mauritania iliwataka watu wasivuke mpaka na “wasisafiri kwenda maeneo yasiyo salama.” Diplomasia ya Mauritania inajitahidi kuepuka kuongezeka mvutano na kudumisha uhusiano wa amani na jirani yake wa Mali. Nchi hizo mbili zilibainisha wiki iliyopita nia yao ya kuimarisha ushirikiano wao.