
Watu ishirini wamefariki kusini mwa Tanzania katika maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa, mamlaka imetangaza siku ya Alhamisi Machi 26, huku mvua zaidi ikitarajiwa. Mvua imekuwa ikinyesha Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa, ambayo mwezi Machi ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 81 na maelfu kuhama makazi yao katika nchi jirani ya Kenya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchini Tanzania, mvua hiyo, pamoja na upepo mkali, ilisababisha maporomoko ya ardhi yaliyoharibu nyumba mapema siku ya Jumatano asubuhi katika mkoa wa Mbeya (kusini), alisema Jaffar Haniu, mkuu wa wilaya ya Rungwe ambapo maafa hayo yalitokea. “Idadi ya vifo sasa imeongezeka hadi 20,” aliwaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa miili 18 ilipatikana siku ya Jumatano na miwili Alhamisi.
“Mmoja wa waathiriwa ni mtoto mdogo sana, mwenye umri wa miezi 18 tu,” Bw. Haniu aliongeza, akiwasihi wakazi wa eneo hilo “kuchukua tahadhari” kwani mvua kubwa bado inatarajiwa. “Wale wanaoishi katika maeneo yaliyo hatarini kuathiriwa na maporomoko ya ardhi wanapaswa kuondoka mara moja hadi hali itakapoboreka,” alibainisha.
Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Tanzania inatabiri mvua kubwa katika sehemu kubwa ya nchi hadi Jumanne ya wiki ijayo.