
Rais wa Marekani Donald Trump ameahirisha makataa yake dhidi ya Iran kabla ya mashambulizi yanayowezekana kwenye mitambo ya umeme hadi Aprili 6
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Donald Trump ametangaza siku ya Alhamisi kwamba anaahirisha makataa yake kabla ya mashambulizi ya Marekani yanayowezekana kwenye vituo vya umeme ya Iran hadi Aprili 6, akihakikisha kwamba mazungumzo na Tehran yanaenda “vizuri.”
“Kwa ombi la serikali ya Iran,” rais wa Marekani alitangaza kwenye mtandao wake wa Truth Social, “Ninasimamisha uharibifu wa vituo vya umeme kwa siku kumi hadi Jumatatu, Aprili 6, saa 2:00 usiku saa za Washington.” Siku ya Jumatatu, Machi 23, alitangaza kusitishwa kwa vitisho vyake vya kushambulia miundombinu ya nishati hadi siku ya Ijumaa, Machi 27.
“Mazungumzo yanaendelea na, kinyume na kile ambacho vyombo vya habari vya uongo vinasema (…), yanaendelea vizuri sana,” rais wa Marekani aliongeza.