
Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kuwa: “Meli kadhaa za kivita za jeshi gaidi la Marekani zimezamishwa majini, na idadi kubwa ya wanajeshi kuuawa katika wimbi la 84 “la Operesheni Ahadi ya Kweli 4.”
Taarifa ya Idara ya Mahusiano ya Umma ya IRGC imesema: “Kufuatia wimbi la 84 la Operesheni Ahadi ya Kweli ya 4, iliyofanyika kwa jina la msimbo la “Yaa Man Huwa Shadidul I’qab”, Jeshi la Wanamaji la IRGC limefanya shambulio mseto dhidi ya magaidi wa Kizayuni-Kimarekani katika Bandari ya Al-Shuyukh na pwani ya Bandari ya Dubai, na kulenga kwa usahihi wanajeshi wa Marekani waliokuwa wamekata tamaa na zana zao za kimkakati.”
Meli 6 za kivita za Marekani za LCU zimepigwa katika Bandari ya Al-Shuyukh katika operesheni hiyo iliyofanywa kwa kutumia makombora ya balestiki na yale ya Cruise aina ya Qadr 380. Kwa mujibu wa ripoti za uwanjani, meli 3 kati ya hizo za kivita zimezamishwa baada ya kupigwa, na zingine zinateketea kwa moto.
Wakati huo huo, Jeshi la Iran limetekeleza operesheni dhidi ya vituo vya mkusanyiko wa maafisa wa jeshi gaidi la Marekani wa kitengo cha ndege zisizo na rubani kwenye ufukwe na mojawapo ya hoteli huko Dubai, kwa kutumia ndege zisizo na rubani, na kusababisha hasara kwenye vituo hivyo.
Katika operesheni hiyo meli za kivita zimezamishwa baharini na idadi kubwa ya magaidi wa Marekani wameuawa. “Tulikuwa tumesema hapo awali kwamba tutakusakeni popote muendapo na kukutieni adabu”, imesema taarifa hiyo ya IRGC.