
Nchi ya Senegal, ni miongoni mwa mataifa 20 ambayo yamekataa jina la rais wa zamani Macky Sall, kuwa mwakilishi wa Afrika kwenye kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchi hizo zinasema, hatua iliyochukuliwa na rais wa Burundi ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Mataifa, hazikuhusishwa kuhusu azma ya rais huyo wa zamani wa Senegal.
Balozi wa Senegal kwenye Umoja wa Afrika, amesema serikali jijini Dakar, haikuhusishwa kuhusu mpango huo wa Sall, ambaye analenga kumrithi Antonio Guteress, ambaye muda wake unaomalizika mwaka huu.
Aidha, Senegal imesisitiza kuwa haijawahi kuidhinisha ugombea wa Sall na haitambui mchakato huo ulioanzishwa na Burundi, ambayo kwa sasa inaongoza Umoja wa Afrika.
Mataifa mengine yanayopinga ugombea wa Sall ni pamoja na Tunisia, Afrika Kusini na Nigeria. Nigeria imesema kumpendekeza Macky Sall kuwania nafasi hiyo, itakwenda kinyume na utaratibu wa nafasi hiyo kuzunguka kwenye mabara, akisema ni fursa ya Latin Amerika na Carribbean kumtoa Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa.