
Maria Zakharova, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, amesema kupitia taarifa akiashiria hujuma za kijeshi za Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kwamba: “Sababu ya mashambulio dhidi ya nchi hii inahusiana moja kwa moja na tamaa ya madola ya kigeni ya kutaka kupora na kudhibiti rasilimali zake za mafuta na gesi.”
Maria Zakharova alisema siku ya Ijumaa kwamba: “mashambulio dhidi ya Iran, Venezuela, na kabla ya hapo Iraq na Libya, siku zote yamekuwa yakihusiana moja kwa moja na rasilimali za mafuta na gesi na uhamishiaji wa rasilimali hizo katika nchi mbalimbali za dunia.” Zakharova ameongeza: “Rasilimali za nishati ndiyo sababu kuu ya kuibuka mivutano na migogoro ya kimataifa katika maeneo haya.”
Hujuma za pamoja za kijeshi za Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran zilianza tarehe 28 Februari mwaka huu; uvamizi ambao ulifanyika wakati mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yalikuwa yakiendelea kati ya Iran na Marekani.