Mahakama ya Katiba nchini Congo-Brazzaville, imethibitisha ushindi wa Denis Sassou Nguesso. Siku ya Jumamosi, Machi 28, Mahakama ya Katiba ilitatua mzozo wa uchaguzi. Ilifutilia mbali ombi la kufuta uchaguzi wa Machi 15, lililowasilishwa na mgombea Dave Mafoula. Kulingana na takwimu rasmi, rais Denis Sassou Nguesso alipata 94.90% ya kura, ikilinganishwa na 94.82% iliyotangazwa hapo awali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Brazzaville, Loïcia Martial

Bila wakili, Dave Mafoula, akiwa amevaa shati na suti bila tai, alishutumu mbele ya Mahakama ya Katiba makosa ambayo anadai kuwa aliyashuhudia wakati wa uchaguzi: kadi za kura kujazwa katika masanduku ya kura, ufisadi, na wapiga kura kubadilishiwa kituo cha kupigia kura katika dakika za mwisho.

Ombi limekataliwa

Ombi limekataliwa na Mahakama. Dave Mafoula amelalamika: “Kwa upande wangu, nilidhani tunaweza kuungana, ili tuweze kutoa kile ambacho Kongo inatarajia kutoka kwa raia wake; kwa sababu nchi ambayo haijaungana, nchi ambayo imegawanyika, nchi ambayo haitaki kusema ukweli, nchi inayotaka kusonga mbele kwa uongo, haiwezi kusonga mbele kikweli.”

Kwa upande wake, Yvon Eric Ibouanga, mmoja wa mawakili wawili wa rais Denis Sassou Nguesso, ameelezea kuridhika na maamuzi ya Mahakama ya Katiba: “Kwetu sisi, utaratibu huu ni msimamo wa mwisho, kwa sababu kila kitu kimewekwa wazi, kila kitu kimechunguzwa. Mjadala ulifanyika kwa umakini. Kwa hivyo, uamuzi huo unaonyesha matokeo yasiyokuwa na upendeleo,” alisema.

Uamuzi usioweza kutenguliwa

Maamuzi ya Mahakama ya Katiba hayawezi kutenguliwa. Kulingana na takwimu rasmi, rais aliye madarakani alipata 94.90% ya kura zilizopigwa. Idadi ya wapiga kura ilikuwa 85.99%. Hatua inayofuata sasa ni kuapishwa kwa rais Denis Sassou Nguesso kwa muhula wa tano mfululizo. Zoezi hilo litafanyika Aprili 16, katika uwanja wa michezo kaskazini mwa mji mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *