Chanzo cha picha, Getty Images
Waasi wa Houthi wa Yemen wanasema wamefanya shambulio la pili katika sehemu za kusini mwa Israeli leo.
Yahya Saree, msemaji wa Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen, kundi la Houthi la jeshi la Yemen, anasema kundi hilo lilifanya “mkusanyiko wa makombora ya meli na ndege zisizo na rubani” kulenga “maeneo kadhaa muhimu ya kijeshi” ya Israel.
Anaongeza kuwa mashambulizi hayo “yaliambatana” na yale ya Iran na operesheni za kijeshi za Hezbollah, na kwamba “limefanikiwa kufanikisha malengo yake”, na kuongeza kuwa kutakuwa na mashambulizi zaidi katika siku zijazo “hadi adui mhalifu atakapoacha mashambulizi na uchokozi wake”.
Taarifa hiyo kwenye akaunti yake ya Telegram inakuja baada ya ripoti katika vyombo vya habari vya Israel na Marekani kuhusu duru ya pili ya mashambulizi ya Houthi, saa chache baada ya Houthi kuthibitisha kuwa walikuwa wamerusha kombora lao la kwanza kuelekea Israel tangu mgogoro na Iran ulipoanza.
Mapema leo, Israel ilisema ilikuwa imezuia kombora lililokuwa likitoka Yemen.
Unaweza kusoma;