Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeendesha Shindano kwa Washiriki kutoka vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu yaani the Capital Markets Universities and Other Higher Learning Institutions Challenge lenye lengo la kujenga uelewa wa masoko ya mitaji na uwekezaji.

Shindano hili limetumia Tekno­lojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ikiwa ni pamoja na mitandao ya kielektroniki yaani simu za mikononi na intaneti. Shindano limegawanyika kati­ka sehemu kuu mbili, ambazo ni (shindano la maswali na majibu – Quiz Competition) na (Shindano la kuandika Insha – Essay Com­petition).

Kupitia shindano hili, katika mwaka 2025, CMSA imeweza kuwafikia washiriki 28,393 ikil­inganishwa na wanafunzi 20,000 waliotarajiwa, na hivyo kuvu­ka lengo la ushiriki na kupata mafanikio kwa asilimia 142. Idadi hii imefanya jumla ya wanafun­zi walioshiriki tangu kuanzish­wa kwa shindano hili kufikia 116,871. Mafanikio haya yameto­kana na jitihada za CMSA katika kuhamasisha wanafunzi kushiri­ki katika shindano hili, pamoja na matumizi ya TEHAMA kwa njia ya simu za mkononi, tovuti, na barua pepe.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, CPA. Nicodemus Mkama akitoa hotuba wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu na mahafali ya wahatimu wa mafunzo ya washiriki katika masoko ya mitaji.

Katika jitihada za kuhakikisha washiriki wanatumia elimu ya nadharia kwa vitendo, Mamlaka imefanikiwa kuweka utaratibu wa kuwawezesha washiriki wa shin­dano hili kuwa wawekezaji hali­si, ambapo washiriki watatumia theluthi moja (1/3) ya fedha walizotuzwa kuwekeza katika hisa za kampuni zilizoorodhesh­wa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam au katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja iliy­oidhinishwa na CMSA.

Kwa mwaka 2024, washindi wa shindano hili waliwezeshwa na CMSA kuwekeza shilingi mili­oni 10 katika makundi mawili, na leo hii uwekezaji wao umeongeze­ka na kufikia shilingi milioni 125 kwa kundi la kwanza; na milioni 128 kwa kundi la pili, sawa na ongezeko la asilimia 1,150 na 1,180 mtawalia.

Serikali yapongeza ukuaji na ust­awi wa Masoko ya Mitaji

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ame­pongeza maendeleo ya masoko ya mitaji nchini Tanzania, akibain­isha kuwa jumla ya thamani ya uwekezaji katika masoko ya mita­ji sasa imefikia Sh 63.1 trilioni. Waziri alisisitiza kwamba ukuaji huu ni matokeo ya moja kwa moja ya sera zinazowezesha uwekeza­ji, usimamizi thabiti, na jitihada za kimkakati kama programu ya elimu kwa umma inayotolewa na CMSA.

Mhe. Waziri alionge­za kuwa Serikali imejikita katika kuunda mazingira yanayoweze­sha uwekezaji, yanayoendana na malengo ya DIRA 2050, kwa lengo la kuimarisha masoko ya fedha na kuchochea ukuaji wa uchumi. Aidha, Mhe. Waziri alibainisha kwamba mafanikio haya yana­onyesha uwezo wa masoko ya mitaji kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha za kugharamia miradi ya maendeleo, kupanua fursa za uwekezaji, na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Serikali yapongeza wataalamu wa Masoko ya Mitaji wenye wele­di na ujuzi kimataifa

Katika jitihada za kuongeza idadi ya wataalamu wa masoko ya mitaji wenye ujuzi na wele­di kwa viwango vya kimataifa, CMSA inashirikiana na Taasi­si ya Kimataifa ya Dhamana na Uwekezaji (Chartered Institute for Securities and Investment – CISI) ya nchini Uingereza, katika kuendesha mafunzo yanayotam­bulika kimataifa. Mafunzo haya yameongeza ujuzi na weledi kwa wahitimu unaowawezesha kuk­abiliana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ya sekta ya masoko ya mitaji na dhamana ulimwenguni.

Katika kutekeleza mkakati huo, CMSA kwa kushirikiana na CISI imeendesha mafunzo kwa watendaji wa masoko ya mita­ji hapa nchini, ambapo Mafun­zo haya yamefanikiwa kupata washiriki 128, ikilinganiswha na lengo la kupata washiriki 80, na hivyo kuvuka lengo la ushiriki kwa kupata mafanikio ya asili­mia 160. Kati ya washiriki 128 wa mafunzo hayo, washiriki 95, sawa na asilimia 74.2 wamefau­lu mitihani inayokidhi viwango vya kimataifa na wamefanikiwa kutunukiwa vyeti na Mhe. Waziri wa Fedha.

Washiriki 12 wa juu wa shindano la masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wakipokea zawadi ya mfano wa tiketi ya ndege kwenda Nigeria kuhudhuria mafunzo kwa vitendo, ikiwa ni moja ya zawadi za washindi wa shindano hilo.

mafunzo haya yamekuwa cha­chu yenye matokeo chanya kwa maendeleo na ustawi wa masoko ya mitaji hapa nchini. Chini ya usimamizi wa CMSA, wataalamu hawa wamewezesha kuanzishwa kwa bidhaa mpya na bunifu kati­ka masoko ya mitaji Tanzania.

Bidhaa hizo ni pamoja na hat­ifungani za kijani yaani green bond, hatifungani za jamii yaani social bond, na hatifungani zenye kukidhi matakwa ya Shariah yaani Sukuk bonds. Matokeo hayo yam­eiweka Tanzania katika ramani ya masoko ya mitaji ulimwenguni yanayotoa bidhaa bunifu zinaz­ovutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini.

CMSA itaendelea kutekele­za mikakati ya kutoa elimu kwa umma na kuendesha mafunzo kwa wataalamu wa masoko ya mitaji wenye ujuzi na weledi kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *