Kamanda wa ngazi ya juu wa vikosi vya ulinzi vya Yemen amesema: Tunatumia chaguo la kufunga Mlango Bahari wa Babul Mandab kwa meli za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Abed al Athawr amesema tupo bega kwa bega na Iran na haturuhusu Bahari Nyekundu itumike kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Amesema Yemen imeingia rasmi katika duru mpya ya mapigano dhidi ya adui Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba mambo mengi ya kushangaza yapo njiani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *