
Chris Murphy Seneta wa chama cha Democratic cha nchini Marekani amesema kuwa uwongo wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo kwamba anafanya mazungumzo na Iran unatoa ujumbe huu kwa Tehran kwamba amekwama kwenye kinamasi na amezongwa na mashinikizo.
Chris Murphy amechapisha tena matamshi ya Jimmy Hyams mjumbe wa ngazi ya juu wa Kundi la Intelijinsia katika Bunge la Wawakilishi la Marekani ambaye katika mahojiano alisema kuwa “Trump anasema uwongo waziwazi kuhusu mazungumzo ya kisiasa na Iran”, na kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kwamba: Uwongo huo umetuma ujumbe muhimu sana kwa Iran kwamba Trump amekwama na amezingirwa.
Seneta huyo Mdemocrat ameongeza kuwa: Kitendo hiki kinadhihirisha utendaji mbaya wa Rais wa nchi katika uga wa usalama wa taifa wa Marekani.
Gazeti la New York Times pia limeandika: Uwezo wa makombora wa Iran bado upo, na wakati huo huo gazeti hilo limeandika kuwa: Kinyume na madai ya mara kwa mara ya jeshi la Marekani na Trump mwenyewe; uwezo wa makombora wa Iran haujapungua; na Iran ingali na uwezo wa kufanya mashambulizi.
Naye Kelly Griego Mtafiti wa ngazi yajuu wa Kituo cha Stimson huko Washington ameliambia gazeti la New York Times kwamba: Zipo ishara kwamba hatukabiliani na upande uliofeli bali tunakabiliana na Iran ambayo inasababisha hasara kubwa ili kusogeza mbele stratejia yake.
New York Times limeandika: Miri Eisin Kanali mstaafu wa Israel pia ameeleza kuwa: Mashambulizi ya Iran dhidi ya maeneo ya Israel na Marekani yataendelea.