Rais wa Marekani sasa anatishia kuchukua mafuta ya Iran na kwenda mbali zaidi na kudhibiti kisiwa cha Kharg, kinachozalisha bidhaa hiyo, wakati huu vita vikiendelea kwa wiki ya nne.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na Jarida la Financial Times, Trump amesema, Marekani ikiamua, inaweza kuchuklua kisiwa hicho kwa urahisi na kwa haraka.

Iran nayo imetishia kushambulia Vyo vikuu vya Marekani kwenye nchi za Mashariki ya Kati pamoja na makaazi ya maafisa wake na wale wa Israeli.

Aidha, kiongozi huyo wa Marekani amesema anaamini mashambulizi ambayo yamekuwa yakiendelea, yamefanikisha mabadiliko ya utawala nchini Iran na kusisitiza kuwa, uongozi wa sasa unataka mkataba ili vita viishe.

Wakati hayo yakijiri, bei ya mafuta imepanda tena siku ya Jumatatu katika soko la kimataifa kwa sababu ya vita vinavypendelea.

Bei hiyo imepanda kwa asilimia tatu ambapo pipa la mafuta sasa linauzwa kwa Dola 119.

Tangu Iran ilipofunga mlango wa Bahari wa Hormuz, meli zinazosafarisha mafuta na gesi kupitia êneo hilo zimekwama na kusababisha kupanda bei kwa bidhaa hiyo kwa sababu ya uhaba wake katika mataifa mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *