
Kesi katika ngazi ya rufaa ya mashabiki 19 kaika fainali ya AFCON— raia18 wa Senegal na Mfaransa mmoja—waliokamatwa baada ya fainali nchini Morocco na kuhukumiwa katika mahakama ya mwanzo kwa uhuni, imeahirishwa tena, wakati huu hadi Aprili 13. Vita vya kisheria, kidiplomasia, na michezo vinaendelea kati ya Senegal na Morocco.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Rabat, François Hume-Ferkatadji
Katika chumba cha mahakama kilichojaa watu katika Mahakama ya Rufaa ya Rabat—jengo jipya lililoko karibu na Uwanja wa Moulay Abdallah ambapo fainali ilichezwa—Washtakiwa wametenganishwa na sehemu nyingine ya chumba cha mahakama kwa skrini zinazofanana na mashrabiya, kwa hivyo jamaa zao hujipinda ili kuwaona na kuwasalimia. Baadhi ya mawakili walijaribukuzungumza na wateja wao.
Lakini kusikilizwa kwa kesi hiyo kulikuwa kwa muda mfupi, kwani jaji alitangaza kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi Aprili 13. Wakili wa shabiki, raia wa Ufaransa, aliyehukumiwa pamoja na mashabiki wa Senegal katika kesi hiyo, akisema kwamba wakili mpya amejiunga na timu yake.
Mtaalamu wa masuala ya sheria aliyekuwepo kwenye kesi hiyo anaona hii kama mkakati wa kuhakikisha kuachiliwa kwa raia huyo Mfaransa mwenye asili ya Algeria mara tu kesi ya rufaa itakapoanza kwa kuwasilisha ombi la kuachiliwa kwa muda mara moja, kwani mteja wake atakuwa karibu kutumikia kifungo chake cha miezi mitatu jela.
Hata hivyo, hili lilimkatisha tamaa kwa Patrick Kalou, mmoja wa mawakili wanaowawakilisha mashabiki 18 wa Senegal, ambaye alisema alikuwa tayari kupambana katika kesi hiyo. “Tumesikitishwa sana kwa sababu tulikuwa tumefikia makubaliano na baadhi ya mawakili wenzangu ambao, waliondoka nchini mwao kuja kuimarisha timu, kama wale waliotoka Italia na London. Kesi imeahirishwa; kwa hiyo jaji ndio anaamua… tutafuata uamuzi wa jaji na kujiandaa kwa tarehe 13.”
Kundi la mawakili wa upande wa utetezi na upande wa mashtaka—hali isiyo ya kawaida kwa aina hii ya kesi—limeimarishwa zaidi, hasa kwa kuwasili kwa wakili kutoka Italia. Hakika, kulingana na wakili wa upande wa utetezi, miongoni mwa mashabiki 18 wa Senegal, washtakiwa wanne wana uraia pacha: Italia, lakini pia Uhispania, Uingereza, na Marekani.