Mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa Televisheni ya CNN ya Marekani ameitaja hatua ya Iran ya kupiga na kuharibu ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya AWACS kuwa ni pigo kubwa kwa uwezo wa anga wa nchi hiyo.

Cedric Leighton amesema katika ripoti yake kwamba: “Kuharibiwa ndege za ujasusi za Marekani za AWACS kumekwamisha uwezo wa nchi hiyo kukabiliana na Iran.”

Cedric Layton ambaye ni kanali wa zamani wa jeshi la Marekani ameongeza: “Kuharibiwa ndege hiyo iliyopigwa na Iran katika Kambi la Jeshi la Anga ya Prince Sultan huko Saudi Arabia ni pigo kubwa kwa uwezo wa ujasusi wa Marekani akisisitiza kuwa kuharibiwa ndege ya ujasusi ya AWACS kunaathiri uwezo wa ndege za kivita za Marekani kulenga shabaha na kukabiliana na ulinzi wa makombora ya Iran.”

Picha kutoka Kambi ya Anga ya Prince Sultan huko Saudi Arabia zinaonyesha uharibifu wa ndege ya kisasa ya Marekani ya AWACS kufuatia shambulio kali lililofanywa na Jeshi la Iran dhidi ya kambi hiyo inayotumiwa na Marekani kushambuli ardhi ya Iran

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *