Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi
ameiambia Saudi Arabia kuwa ni “wakati umefika wa kuyaondoa majeshi ya
Marekani’’ nchini mwao.

Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Araghchi
anasema Iran “inaiheshimu” Saudi Arabia na inaiona kama “taifa
ndugu”.

Operesheni za Iran zinalenga “wachokozi wa
maadui ambao hawana hawawaeshimu Waarabu au Wairan”, anasema.

Araghchi alichapisha maoni yake pamoja na picha
inayoonekana kuonyesha ndege iliyoharibiwa na iliyo na alama za Jeshi la Anga
la Marekani. “Angalia tu kile tulichofanya dhidi ya kamandi yao ya
anga,” anaandika.

Kamandi Kuu ya Marekani bado haijatoa kauli yoyotehadharani
kuhusu tukio hilo. BBC imewasiliana na wahusika kupata maoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *