Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kuzuru nchini Syria, ofisi ya rais wa Syria imetangaza siku ya Jumapili Julai 5, bila kutaja tarehe ya ziara yake, ambayo itakuwa ya kwanza kufanywa na mkuu wa nchi ya Magharibi tangu Rais Ahmad Al-sharaa aingie madarakani mwishoni mwa mwaka 2024.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa nchini Syria tangu Nicolas Sarkozy alipozuru nchi hii mnamo mwaka 2008-2009, kabla ya nchi hizi kuvunja mahusiano kutokana na ukandamizaji mnamo mwaka 2011 uliotekelezwa na utawala wa Bashar al-Assad. Emir wa Qatar na Rais Volodymyr Zelensky walizuru Syria baada ya kuanguka kwa Assad.

Mnamo Mei 2025, Bw. Macron alimpokea Rais wa Syria Ahmad Al-sharaa, kiongozi wa zamani wa kuni la wanamgambo wa Kiislamu aliyechukua madaraka huko Damascus, na aliahidi kushinikiza Umoja wa Ulaya na Marekani kuondoa vikwazo vikali vilivyowekwa dhidi ya Syria, ambavyo vingi vimeondolewa tangu wakati huo.

Ikuu ya Élysée haijasema lolote kuhusu ziara hii ya rais Macron nchini Syria.

Shirika la habari la serikali ya Syria, SANA, likinukuu ofisi ya Bw. Al-sharaa, halikutoa maelezo kuhusu tarehe ya ziara ya Bw. Macron. Hata hivyo, rais wa Ufaransa atahudhuria mkutano wa kilele wa NATO mjini Ankara, Uturuki, siku ya Jumanne na Jumatano.

Bw. Macron ataambatana na wawekezaji na wawakilishi wa makampuni ya Ufaransa, SANA imeripoti.

Mgogoro wa miaka 14 nchini Syria umewaua karibu watu nusu milioni na mamilioni ya watu kuyahama makazi yao. Miundombinu ya Syria imeharibika, na ingawa nchi na makampuni mengine yameahidi uwekezaji mkubwa, nchi hiyo bado inahitaji mamia ya mabilioni ya dola ili kujejinga upya na kuwatoa mamilioni kutoka katika umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *