Gazeti la Uingereza la The Guardian limeandika katika ripoti yake kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimetoa mashinikizo makubwa kwa Wamarekani na kuongeza pakubwa gharama za maisha yao ya kila siku.

The Guardian limeongeza kuwa: “Baada ya hujuma ya Wamarekani na Wazayuni dhidi ya Iran, hali ya taharuki kubwa imetanda katika masoko ya kimataifa, ikiongeza bei za mafuta, vyakula, mbolea za kemikali na mikopo ya nyumba.” Gazeti hilo la Uingereza limeeleza kuwa, mashinikizo hayo ya kiuchumi yameongezeka kufuatia jibu kali la Iran kwa mashambulizi ya Marekani na Wazayuni na kufungwa Lango Bahari la Hormuz linalohesabiwa kuwa njia muhimu sana ya uchukuzi duniani. Linasema hali hii imewafanya Wamarekani kufikiria upya matumizi yao ya kila siku na kuweka akiba ya chakula pamoja na kubana matumizi ya umeme na nishati ili kupunguza shinikizo la kiuchumi.

Mfanyakazi mmoja wa benki huko Indianapolis, Marekani, amekiri kwamba huenda asiweze kumudu kutumia gari lake siku za usoni kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na kwamba hatakuwa na pesa za kulirekebisha iwapo litahitajia marekebisho. Wakati huohuo, mfanyakazi mwingine wa maktaba huko Massachusetts, Marekani, amesema yeye na mke wake wamelazimika kufanya kazi zamu za jioni kutokana na kupanda kila siku kwa gharama za maisha na usafiri, lakini pamoja na hayo bado hawawezi kumudu gharama hizo. Amesema kwa uchungu: “Tunazama. Kiasi hiki cha kazi na mashinikizo hakivumiliki na kinadhuru afya zetu za kimwili na kiakili.”

Kuhusu kizazi kipya cha Marekani kutoamini mkakati wa Trump dhidi ya Iran,

gazeti la The Guardian limeandika kwamba vijana wa kihafidhina wa Marekani wanatilia shaka siasa za Rais Donald Trump wa Marekani wakisema wamesikitishwa na uamuzi wa Donald Trump wa kuanzisha vita dhidi ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *