
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Marco Rubio amesema Washington italazimika kuangazia upya uhusiano wake na muungano wa NATO baada ya vita vyake dhidi ya Iran kumalizika.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Licha ya kuweka wazi kwamba Marekani itaangazia upya ushirikiano wake na NATO, uamuzi wa mwisho utafanywa na Rais Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump amezituhumu nchi washirika wake kwa kushindwa kusaidia katika juhudi za Washington kuufunga mlango wa bahari wa Hormuz uliofungwa na Iran.
Rubio aidha amesisitiza kwamba Washington haijazitaka nchi za NATO kutekeleza mashambulio dhidi ya Iran lakini nchi hizo zimekuwa zikiizuia Marekani kutumia kambi zake za kijeshi licha ya kwamba Washington ni nchi mwanachama wa NATO.
“Nadhani hakuna shaka kwamba baada ya vita hivi kukamilika, tutaufanyika uhusiano wetu na NATO tathmini. Tutaangazia umuhimu wa NATO kwa ushirikiano wake na nchi yetu. ” Alisema Marco Rubio.
Matamshi ya Rubio yamejiri baada ya nchi kadhaa za Ulaya kuizuia Marekani kutumia kambi zake za kijeshi wakati huu vita vyake na Iran vikiendelea.
Mapema Jumanne, Italia iliripotiwa kuzuia ndege za Marekani kutua kwenye ardhi yake wakati ikielekea mashariki ya kati kwa oparesheni.
Nayo Uhispani, Jumatatu ya wiki hii ilitangaza kuzuia ndege za kivita za Marekani kutumia anga yake kusafirisha silaha za kutumika katika vita vya Iran.