#HABARI: Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tabora imetoa mbuzi wanne kama zawadi kwa mashindano ya michezo yanayoendelea katika Gereza Kuu la Uyui, lililopo wilayani hapo na Mkoa wa Tabora ikiwa ni njia ya kuhamasisha ushiriki, nidhamu, mshikamano na kuimarisha afya za wafungwa na mahabusu.

Vilevile, magereza wamekabidhiwa madaftari kwa ajili ya kusaidia shughuli za elimu.

Aidha, Mwenyekiti wa kamati hiyo Upendo Wella ameongoza utoaji wa sadaka ya Sikukuu ya Pasaka katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Igambiro, Kata ya Misha, Tabora Manispaa, kwa lengo la kusaidia ustawi wa watoto hao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *