Jeshi la Burkina Faso na washirika wake pamoja na makundi ya kijihadi, yamewauwa watu 1,800 tangu mwaka 2023 katika vitendo vinavyoelezwa kuwa ni uhalifu wa kivita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti hiyo iliyochapishwa siku ya Alhamisi, Human Rights Watch inasema uongozi wa kijeshi unaoongozwa na Kaptain Ibrahim Traore ulioingia madarakani tangu Septemba 22, mpaka sasa umeshindwa kumaliza visa vya utovu wa usalama, vinavyosababishwa na makundi kama Al-Qaeda na Islamic State.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, jeshi linawategemea raia wanaojitolewa katika mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi na pamoja na makundi hayo, yamesababisha vifo vya watu 1,837 katika majimbo 11 kati ya Januari 2023 hadi Agosti mwaka 2025.

Watoto ni miongoni mwa watu waliouawa katika mashambulizi 57 yaliyotekelezwa na makundi mbalimbali ikiwemo mfano wa kundi la JNIM Agosti mwaka 2024, kuwauwa watu 133 kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine 200 katika mji wa  Barsalogho.

Human Rights Watch inataka Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuanza uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita nchini Burkina Faso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *