
Nchini Haiti, mpango wa kutumwa kwa Kikosi cha kupambana dhidi ya Magenge (FRG) umeanza kutekelezwa. Ujumbe wa kwanza kutoka Chad umewasili mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince tangu siku ya Jumatano, Aprili 1, 2026, ukiambatana na mratibu wa ujumbe huo, Jack Christofides, wiki mbili baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Kenya. Kulingana na FRG, hadi wanajeshi 5,500 watatumwa katika mji mkuu wa Haiti ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Port-au-Prince, Peterson Luxama
Baada ya kushindwa kwa ujumbe wa Ujumbe wa Usaidizi wa Usalama wa Kimataifa , kikosi kipya kinajiandaa kuchukua nafasi ya ujumbe huo nchini Haiti. Kikosi cha kipambana dhidi ya magenge kinaanza kuchukuwa nafasi. Kuwasili Jumatano, Aprili 1, kwa kikosi cha awali cha takriban wanajeshi 50 wa Chad kunaashiria mwanzo wa operesheni hii mpya ya usalama.
Kikosi hiki kinakusudiwa kuchukua nafasi ya Ujumbe wa Usaidizi wa Usalama wa Kimataifa , ambapo matokeo yake yalionekana kuwa machache kwa Wahaiti wengi.
Malengo ya kikosi hiki yako wazi: kufanya kazi kwa ushirikiano na Polisi wa Haiti na Vikosi vya Jeshi ili kuangamiza magenge yenye silaha kupitia shughuli za kijeshi zinazoongozwa na ujasusi, kulinda miundombinu ya kitaifa na barabara kuu, na kulinda raia kwa kuzingatia haki za binadamu.
Jumla ya wanajeshi 5,500 wanatarajiwa
Kikosi cha kupambana dhidi ya magenge kitafanya kazi kwa usaidizi wa Ofisi Jumuishi ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti na Shirika la Mataifa ya Amerika. Hatimaye, vikosi kadhaa vya kigeni kutoka Afrika, Karibiani, na Asia vinatarajiwa kufikia jumla ya wanajeshi 5,500.
Lakini misheni hii mpya inakuja katika muktadha wa wasiwasi hasa. Licha ya hatua zilizowekwa tayari, magenge yanaendelea kulazimisha utawala wao katika vitongoji kadhaa vya mji mkuu na katika baadhi ya miji ya mkoa, kama vile katika eneo la Artibonite.
Katika mji mkuu wa Haiti, raia wanajiuliza ikiwa kikosi hiki kipya kitaweza kutoa matokeo halisi ambapo misheni ya kimataifa inayoongozwa na Kenya ilishindwa.