Hatimaye Balozi wa nyumba 10 katika Mtaa wa Afya, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro wilayani Geita, Cosmas Juakali amerejea kutoka mafichoni baada ya kujificha tangu Novemba mwaka jana, akihofia usalama wake kutokana na sababu za kisiasa, huku familia yake ikitengwa na jamii.

Juakali alivuliwa uongozi kutokana na mgogoro unaodaiwa kusababishwa na fitina za kisiasa kati yake na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa, ambapo sasa amerejeshwa kwenye nafasi yake ya ubalozi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *