Wakiristo kote duniani, wanaadhimisha sikukuu ya Pasaka, kukumbuka kusulubiwa, kufa na kufufuka kwa Mwokozi wao Yesu Kristo, wakati huu dunia ikishuhudia vita kwenye nchi za Mashariki ya Kati.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kiongozi wa Kanisa la Katoliki duniani Papa Leo wa kumi na nne, akiongoza misa ya Pasaka mjini Vatican, ametoa wito kwa mataifa yaliyoanzisha vita vinavyoendelea kuchagua amani, ili irejee kwenye eneo la Mashariki ya Kati.
Kipekee, Papa Leo wa Kumi na nne, ametoa wito kwa rais wa Marekani kutafuta suluhu ya mashambulizi ya nchi yake na Israeli yanayoendelea kutikisa nchi ya Iran, tangu mwezi Februari.
Mjini Jerusalem nchini Israeli, kulikuwa na ukimya huku mji huo ukibaki mahame, kwa sababu ya mashambulizi ya makombora ambayo yamekuwa yakirushwa kutoka Iran.
Nchini Lebanon, hali Kusini mwa nchi hiyo, ambayo imekuwa ikishuhuhudia mashambulizi kutoka kwa Israel wanaowalenga Hezbollah, Wakiristo walisalia nyumbani.
Huko Dubai katika nchi ya Falme za Kiarabu, ibada za kusherehekea Pasaka ziliahirishwa kwa sababu za kiusalama, huku serikali nchini Syria, ikiweka vikwazo kwa ibada kufanyika kwa muda mfupi katika mji wa Damascus.