Chanzo cha picha, US Air Force via Getty Images
“TUMEMPATA!”
Hivi ndivyo Donald Trump alivyoanza chapisho lake
la mtandao wa kijamii akitangaza kuokolewa kwa rubani wa pili wa nMarekani.
Trump anadai hatua hiyo kama ushindi mkubwa kwa
jeshi la Marekani, na kugeuza ktukio ambalo lilizua hofu kuwa sababu ya
kusherehekea.
Kwa muda wa saa 48, alikuwa amekabiliwa na kibarua
kigumu cha kumuokoa rubani wa ndege ya kivita ya Marekani, ambaye sasa tunafahamishwa
alikuwa kanali, alikamatwa na Iran na uwezekano mkubwa kuonyeshwa kwenye
televisheni ya serikali.
Majukwaa ya mitandao ya kijamii yanayoiunga mkono
Irani hapo awali zilichukua fursa ya tukio hilo kuelezea kinachofanyika Iran.
Baadhi walichapisha video ya rubani huyo akifukuzwa
na wenyeji, huku wengine wakiweka mtandaoni picha za Akili Mnemba za afisa huyo
akifurahia ukarimu wa Iran.
Msemaji wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa ameiita siku ya “kufedhehesha” kwa Marekani.