Waziri Mkuu wa Uhispania amesisitiza kuwa nchi hiyo haitadanganywa tena na Marekani kuhusu vita dhidi ya Iran.

Pedro Sanchez, Waziri Mkuu wa Uhispania, huku akizungumzia uzoefu mchungu wa uvamizi wa kigeni dhidi ya Iraq mwaka 2003, amekariri kwamba nchi yake haitadanganywa na ahadi za Marekani za eti kudhamini usalama kupitia uingiliaji wa kijeshi. Amesisitiza sera ya serikali ya Madrid ya kupinga vita, na kusema msimamo wa serikali yake unaweza kufupishwa kwa maneno machache yafuatayo: “Hapana kwa vita.”

Akizungumzia uzoefu uliopita, amesema: “Dunia, Ulaya na Hispania pia zilikabiliwa na hali kama hii huko nyuma.” Sanchez ameongeza kuwa: “Miaka 23 iliyopita, utawala wa wakati huo wa Marekani ulituingiza katika vita Asia Magharibi, ambavyo vilidaiwa kuwa vinalenga kuharibu silaha za maangamizi za Saddam, kueneza demokrasia na kudhamini usalama.”

Baada ya kupita muda, ikadhihirika wazi kwamba matokeo ya vita hivi yalikuwa kinyume kabisa ambapo badala ya kuleta usalama, yalisababisha wimbi kubwa la ukosefu wa usalama barani Ulaya; kwa namna ambayo hali hii inachukuliwa kuwa mojawapo ya machafuko makubwa zaidi ya usalama katika bara hili tangu kuporomoka kwa Ukuta wa Berlin. Awali alisema katika swali muhimu la kuhoji uchokozi haramu dhidi ya Iran kwa kusema: “Je, haya yote yanafanyika kwa lengo gani?” Kudhoofisha sheria za kimataifa, kuyumbisha Asia Magharibi, kuibua migogoro nchini Iraq na Lebanon, na kuizika Gaza chini ya vifusi vya sahau na kutojali.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *