
Nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, sasa itawapokea wahamiaji kadhaa waliofukuzwa kutoka Marekani, mpango utakotekelezwa chini ya makubaliano mapya kati ya utawala wa Kinshasa na Washington.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Serikali ya Kongo inasisitiza kwamba huu si mpango wa kudumu wala utoaji wa sera ya uhamiaji ya Marekani, ambapo watu wanaohusika na mpango huu watapewa hifadhi ya muda mfupi tu.
Tangazo hilo la serikali linasema Kila kesi itapitiwa kwa namna binafsi, kulingana na sheria ya DRC na mahitaji ya usalama wa taifa na kwamba hakutakuwa na uhamisho wa moja kwa moja utakaoidhinishwa.
Hata hivyo asasi za kiraia bado hazijaukaribisha mpango huu zikisema unaashiria ukosefu wa uwazi katika makubaliano haya.