Imekuwa mwezi mmoja tangu AFC/M23 itangaze kuachiliwa kwa takriban wanajeshi 5,000 wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC), kulingana na takwimu zake, au 2,700 kulingana na vyanzo vingine. Wangekabidhiwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na kisha kwa serikali ya Kongo. Lakini tangu tangazo hilo litolewe, hakujawa na maendeleo yoyote.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) iliwasiliana na kueleza utayari wake wa kuunga mkono mchakato huo. Wiki chache zilizopita zimekuwa za wasiwasi, kabla ya utulivu kuonekana katika siku za hivi karibuni. AFC/M23 imeongeza shinikizo lake, hata ikiishutumu Kinshasa kwa kukataa kuwachukua wanajeshi hawa. Kwa upande wa Kinshasa bado inatlia shaka tangazo hilo.

Baadhi ya maafisa wa DRC hata wana hofu ya mkakati wa “kujipenyeza” kwa wapiganaji wa AFC/M23. “Kwa nini wanasisitiza?” “Je, wanafanya kwa nia njema, au wana ajenda iliyofichwa?” anauliza mshirika wa karibu wa Rais FĂ©lix Tshisekedi. Maafisa wengine, wanaoona mbali, lakini ambao bado wangali makini, wanaeleza kwamba hawa ni wafungwa wa vita, na kwamba suala hilo limekuwa likijadiliwa kwa karibu miezi sita.

Kuheshimu taratibu

Waziri mmoja ameiambia RFI kwamba ni muhimu kila kitu kifanyike kwa mujibu wa taratibu. Kulingana na taarifa zetu, mpango upo, lakini hakuna ratiba ya utekelezaji ambayo bado imekamilika. Chanzo cha kidiplomasia kinabainisha kwamba, hata kama makubaliano yatafikiwa kati ya pande hizo mbili, vikwazo vya kifedha vinaweza kuchelewesha mchakato.

Suala hilo linaweza kushughulikiwa ndani ya siku zisizozidi kumi, katika mkutano uliopangwa chini ya upatanishi wa Qatar. Wakati huo huo, wanajeshi hawa wanabaki chini ya jukumu la AFC/M23. Wengi wanakataa kujiunga na tawi la wapiganaji wa AFC/M23 walio katika uwanja wa vita na kwa sasa wanaonekana kama mzigo mkubwa kwa kundi hilo, hasa katika suala la kuwapa chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *