
Marekani inawataka raia wake kufikiria tena kuzuru Nigeria, kwa sababu za kiusalama, kutokana na matukio ya ugaidi, machafuko na utekaji.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii ni taarifa ya hivi punde iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani, ambayo imesema majimbo mbalimbali nchini Nigeria sio salama na mashambulizi yanaweza kutokea sokoni, hotelini au katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu.
Aidha, Washington imeatoa wito kwa raia wake wanaofanya kazi kwenye ubalozi wake jijini Abuja, wasio na kazi za dhararyra, kuondoka na familia zao kwa sababu ya hali mbaya ya usalama nchini Nigeria.
Hatua hii ya Marekani inakuja, wakati huu matukio ya mashambulio yakiendelea kuongezeka ambapo siku chache zilizopita , watu wenye silaha waliwauwa watu zaidi ya 50 katika jimbo la Niger, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Tangazo hili linakuja, licha ya Marekani na Nigeria kuwa na ushirikiano wa ulinzi na usalama kupambana na makundi ya kijihadi na ugaidi, likiwemo kundi la Boko Haram.