Makubaliano dhaifu kati ya Iran na Marekani yanaingia siku yake ya pili leo Alhamisi, huku jumuiya ya kimataifa ikiwa na wasiwasi kwamba mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya Lebanon yanaweza kukwamisha mchakato mzima. Makamu wa Rais J.D. Vance, ambaye anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Marekani katika mazungumzo na Iran nchini Pakistan siku ya Jumamosi, amesema ni juu ya viongozi wa Iran kuamua kama makubaliano hayo yatavunjika kwa sababu ya Lebanon.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon yanaleta “hatari kubwa” kwa usitishaji mapigano wa wiki mbili kati ya Marekani na Iran, ameonya msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumatano. Mashambulizi ya anga ya Israel katika vitongoji vyenye watu wengi katika mji mkuu yamewaua watu wasiopungua 182.

Siku ya Jumatano, jeshi la Israel lilifanya “shambulio lake kubwa zaidi lililoratibiwa” dhidi ya kundi la Hezbollah linalounga mkono Iran, na hivyo dhidi ya Lebanon, bila kuwaonya raia. Kulingana na Wizara ya Afya ya Lebanon, mashambulio haya, yenye vurugu zaidi tangu kuanza kwa vita, yamesababisha vifo vya watu kadhaa na mamia kujeruhiwa. Wizara ya Afya imelaani “kuongezeka kwa hatari.”

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitangaza siku ya Jumatano kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Washington na Tehran hayaonyeshi “mwisho wa kampeni dhidi ya Iran,” na kwamba Israel iko “tayari kuanza tena mapigano wakati wowote.” Kwa upande wake, spika wa bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, aliona kusitisha mapigano na mazungumzo na Marekani kuwa “hayana mantiki,” akibainisha kwamba kanuni tatu kati ya kumi ambazo nchi yake iliziainisha kama msingi wa makubaliano hayo ya amani tayari “zimekiukwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *