.

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa
Marekani Donald Trump ameishutumu Iran kwa “kushughulikia vibaya” meli
za mafuta zinazopita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz, akisema “sio
makubaliano tuliyo nayo”.

Maoni hayo
yanaonyesha udhaifu wa makubaliano ya kusitisha mapigano, huku ripoti
zikionyesha migongano kuhusu kile kilichojumuishwa katika makubaliano hayo.

Hili
limewadia huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema serikali yake inaanza
mazungumzo ya moja kwa moja na Lebanon, ikizingatia Hezbollah kuweka chini
silaha zao, kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na Iran, na kuanzisha
uhusiano wa amani.

Afisa wa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alithibitisha kuwa ataandaa mkutano wiki
ijayo huko Washington “kujadili mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha
mapigano na Israel na Lebanon”.

Maafisa wa
Lebanon walikuwa wameomba kusitisha mapigano kabla ya mazungumzo kuanza, lakini
Netanyahu alisema katika hotuba iliyofuata kwa wakazi wa kaskazini mwa Israeli: “Hakuna kusitisha mapigano nchini Lebanon.”

Baada ya
mashambulizi ya Israeli kuendelea huko Lebanon Alhamisi nzima – yakilenga kile
ilichokielezea kama maeneo ya kurusha roketi za Hezbollah upande wa kusini
– mashambulizi yalionekana kupungua kwa muda usiku kucha katika eneo
hilo.

Trump
alisema katika mahojiano kwamba Israeli “itapunguza” mashambulizi
yake Lebanon ili kuunga mkono mazungumzo ya amani.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *